Habari za Kimataifa

Upinzani Cameroon wajitangazia ushindi

Maurice Kamto

Mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa Cameroon Maurice Kamto anadai kuwa ameshinda uchaguzi wa uraisi wa siku ya jumapili licha ya onyo la serikali dhidi ya hatua hiyo.

Kamto ambaye ni kiongozi wa chama cha Rebirth of Cameroon (MRC), ametoa wito kwa rais Paul Biya kuachia madaraka kwa amani.

Akizungumza na waandishi wa habari mji mkuu wa Yaounde amesema ”Namuomba rais anayeondoka kupanga namna ya kumpokeza madaraka mpizani wake kwa amani.”

Mgombea huyo wa upinzani hakutoa matokeo ya kuthibitisha madai yake japo wafuasi wake walimshangilia kwa vifijo wakati alipokua akitoa tangazo hilo.

Uchaguzi huo umeonekana na wenga kama mpango wa kurefusha utawala wa rais Biya ambaye ni mmoja wa viongozi wa Afrika waliyoshikilia madaraka kwa muda mrefu.

Naibu katibu mkuu wa wa chama tawala cha Cameroon People’s Democratic Movement, Gregoire Owona, amemshutumu Kamto kwa uvunjaji sheria.

“Kamto hakuweka mawakala wake katika kila kituo cha kupiia kura, kwa hivyo ni vigumu kwake kuhesabu kura zote.”

Kwa mujibu wa sheria , kila kituo cha kupigia kura lazima kiwasilishe matokeo yake kwa tume ya uchaguzi ili idhinishe kwamba ni matokeo halisi.

Ni mahakama ya kikatiba pekee iliyo na mamlaka ya kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi katika muda wa siku 15.

Kabla ya uchaguzi mkuu, Kamto alibuni muungano na chama kidogo cha People’s Development Front (FDP) lakini wadadisi wa kisiasa walisema hana uwezo wa kumuondoa madarakani raisi Paul Biya.

Huku hayo yakijiri, mgombea mwingine wa upinzani wa kiti cha urais kwa mara ya kwanza Joshua Osih, wa chama cha SDF amejigamba kuwa ni yeye tu aliye na uwezo wa kutatua matatizo ya Cameroon ndani ya siku 100.

Kuna jumla ya wagombea tisa wa nafasi ya urais katika uchaguzi huo mkuu wa Cameroon,huku taifa hilo likionekana kuwa na mgawanyiko mkubwa kwa misingi ya lugha.

Maafisa wa tume ya uchaguzi wana hadi wiki mbili kutangaz rasmi matokeo ya uchaguzi huo ambao ulivurugwa katika maeneo mengine na kundi la wanamgambo wanaopigania kujitenga kwa maeneo yanayokaliwa na watu wanaozungumza lugha ya kiingereza.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close