Home / Habari Za Kitaifa / *MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA KILIMANJARO AHAMASISHA WAZAZI*

*MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA KILIMANJARO AHAMASISHA WAZAZI*

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA KILIMANJARO AHAMASISHA WAZAZI

Tarehe 25/10/2018, *Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Chief Daudi Babu Mwidadi Mrindoko*, alialikwa kwenye Mahafali ya 12 ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Kibororoni ambapo alialikwa kama Mgeni wa Heshima.

Katika Mahafali hiyo Ndugu *Chief Mrindoko* aliwahamasisha wazazi washiriki kwenye michango ya hiari waliyokubaliana kwenye vikao; ambapo michango hiyo ni pamoja na michango ya Chakula na michango ya maendeleo ya shule.

Pia *Chief Mrindoko* aliwashauri Wazazi Wajenge jengo la kidato cha 5 na 6 pamoja na jengo la utawala la shule hiyo; ili shule hiyo ianze kupokea wanafunzi wa kada hiyo na pamoja na wanafunzi wanao hitimu kidato cha 4 waweze kurudi kujiunga tena kidato cha 5 na 6.

*kwakuonyesha mfano Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa kilimanjaro Alitoa Kiasi cha Fedha ya kununua nusu � tani ya Cement kwa ajili ya kuanza ujenzi huo*.

*Ndugu Chief Mrindoko aliwaambia kuwa suala la Maendeleo ya shule lisiachiwe Serikali peke yake kwani wazazi nao pia wana nafasi yao katika kichangia maendeleo ya shule na elimu ya watoto wao*.

Katika Mahafali hiyo *Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Maji safi, taka na Mazingira (MUWSA) ambaye aliwakilishwa na Afisa Mahusiano wa MUWSA Ndugu Rashidi Alisema kuwa wao watashirikiana na wazazi pamija na uongozi wa shule hiyo katika ujenzi huo na kwakuanza #watatoa tofali elfu mbili (2000)* kwaajili ya ujenzi wa vyoo pamoja na jengo la utawala huku *Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Eng Masalu Dede akiunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki tano (500,000)*.

Mwisho Mwenyekiti Chief Mrindoko aliwashukuru sana Waalimu na Bodi kwa kumualika na kiwapongeza wanafunzi kwa kuonyesha uwezo wao wa masomo na michezo na kuwaambia *”Elimu ndiyo Maisha na Maisha ndiyo Elimu”*

Imetolewa ma Jumuiya ya Wazazi Mkoa Kilimanjaro
27/10/2018

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *