Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L’Equipe, kupitia Express)
Real Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na Barcelona Jumapili. (Sun)
- Mourinho: Ronaldo hatahamia Manchester United
- Ibrahimovic awafikia Ronaldo na Messi
- Ronaldo aomba simu na kujiangalia uwanjani
Mazungumzo ya Real na kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ya kumtaka achukue mikoba ya ukufunzi Madrid yamekwama. Hii ndiyo sababu iliyochangia Santiago Solari ambaye ni mkufunzi wa timu ya akiba kuwekwa kwenye usukani. Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu pia kumrithi Lopetegui. (Marca)

Antonio Conte
Besiktas wanataka kumrejesha kipa wa Liverpool Loris Karius kwa klabu hiyo ya Anfield. Kocha huyo alitia saini mkataba wa mkopo wa miaka miwili na klabu hiyo ya Uturuki.
Wanataka Mjerumani huyo arejee Anfield mwezi januari na badala yake wakabidhiwe mshambuliaji Mbelgiji mwenye asili ya Kenya Divock Origi, 23. (90 Minutes)
Meneja Jose Mourinho ataungwa mkono Januari kuwanunua wachezaji zaidi kuimarisha kikosi cha Manchester United iwapo atawapata wachezaji wafaao. Inadaiwa kwamba ametengewa kitita cha karibu £100m. (Guardian)
Mwanawe Vichai Srivaddhanaprabha, Aiyawatt, aliyekuwa wa kwanza kumhoji meneja Claudio Ranieri aliyewasaidia kushinda Ligi Kuu ya England kabla yake kuteuliwa rasmi, anatarajiwa kuongoza Leicester baada ya babake kufariki katika ajali ya helikopta iliyoua babake na watu wengine wanne. (Mail)
Lopetegui: Gareth Bale ‘atajaza pengo’ la Ronaldo
Sababu ya Ronaldo kuorodheshwa wa 49 duniani
Mshambuliaji wa Barcelona anayechezea Ufaransa Ousmane Dembele huenda akaruhusiwa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. Chelsea, Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa na kutaka kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Sun)
Juventus wanataka sana kumnunua beki wa miaka 21 kutoka Serbia Nikola Milenkovic, ambaye anadaiwa pia kunyatiwa na Tottenham na Manchester United. Juve pia wanamtaka kiungo wa kati wa Italia Federico Chiesa, 21, lakini Fiorentina huenda wakataka kulipwa zaidi ya euro 100m (£89m) ndipo wakubali kuwaachilia wawili hao. (Calciomercato)
Meneja wa zamani wa Aston Villa Steve Bruce anahusishwa na kuhamia Reading. Klabu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya 22 kwenye liig ya wakiwa na Paul Clement. (Birmingham Mail)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe amemhakikishia mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England Jermain Defoe kwamba bado anahitajika Bournemouth, licha ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 kuchezeshwa mara tatu pekee Ligi ya Premia, wakati wote akiingia kama nguvu mpya. (Mirror)
Manchester United hawajawasiliana na mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Paul Mitchell kuhusu kuhudumu katika nafasi kama hiyo ambayo wanapanga kuianzisha Old Trafford. Hata hivyo, mkuu huyo wa zamani wa usajili wa wachezaji Tottenham anafurahia kuhusishwa na kazi hiyo. (Sun)
Kiungo wa kati wa Liverpool kutoka Brazil Fabinho, 25, anasema amekubwa na matatizo katika kujaribu kuzoea maisha mapya tangu alipohamia Anfield kutoka Monaco kwa £39m majira yajoto. (ESPN)
Winga wa Lyon na Uholanzi aliyewahi kuichezea Manchester United Memphis Depay, 24, amedai kwamba hajajihisi kama mchezaji anayeheshimiwa. (ESPN)
Meneja wa Rafael Benitez amesisitiza kwamba Newcastle ni mkosi tu unaowaandama na si kwamba hawachezi vyema kwenye mechi zao za karibuni. Vijana hao wameshindwa kushinda mechi hata moja kati ya kumi za kwanza walizocheza msimu huu. (Newcastle Chronicle)
Meneja wa Aston Villa Dean Smith anapanga kuwasilisha ofa ya £8m kutaka kumnunua mchezaji kiungo wa kati wa Scotland anayechezea Sheffield Wednesday Barry Bannan, 28, arejee katika klabu hiyo.(Mirror)
Bora kutoka Jumatatu
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameonya Real kuwa wana uwezekano mdogo wa kumchukua Mauricio Pochettino kutoka Tottenham kuchukua mahala pake Lopetegui. (Evening Standard)
Makamu wa rais wa Juventus Pavel Nedved amekana madai ya kumsaini tena kiungo wa kati wa Manchester United mfaransa Paul Pogba, 25. (Sky Italia, kupitia Inside Futbol)
Manchester United na Chelsea wanatarajiwa kushindania kumsaini kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27. (Express)
Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Croatia Mateo Kovacic, 24, aliyekuwa kwenye mkopo kutoka Real Madrid anasema ni mapema sana kuzungumzia kuhama kabisa lakini anasema anafurahishwa sana na maisha ya London. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, hajawahi kufurahia kuwa mchezaji wa ziada hata wakati alikuwa na umri wa miaka mitano, kwa mujibu wa kocha wake wa zamani. (Mirror)