Home / Habari za Kimataifa / Kwa miaka 40 fuvu la Mangi Meli kutoka Tanzania limekuwa likitafutwa nchini Ujerumani

Kwa miaka 40 fuvu la Mangi Meli kutoka Tanzania limekuwa likitafutwa nchini Ujerumani


Shinikizo zinazidi kuongezeka nchini Ujerumani na Uingereza za kutaka kurejeshwa mafuvu yaliyotelewa Afrika kwa utafiti zaidi ya karne moja ikiyopita.

Raia wa Tanzania anayeishi nchini Ujerumani Mnyaka Sururu Mboro, amekuwa akitafuta fuvu lililotoweka la Mangi Meli kwa miaka 40.

Mangi Meli chifu kutoka eneo la kaskazini ambalo kwa saa ndiyo nchi ya Tanzania aliuawa mwaka 1900 kwa wajibu wake wa kuasi dhidi ya utawala wa ukoloni wa Ujerumani.

Baada ya kuuawa mwili wake uliakatwakatwa na kichwa chake kikasafirishwa kwenda nchini Ujerumani.

Lilipo fuvu lake bado haijulikani, lakini baada ya wakfu unaofahamika kama Prussian Cultural Heritage wa mjini Berlin kugundua mafuvu zaidi kutoka Tanzania, imempa Bw Mboro na matumaini mengi.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga amesema serikali inataka kujadili kurejeshwa mabaki hayo.

Maziko mazuri ndicho kilicho akilini mwa Bw Mboro.

Anasema kuwa ikiwa atarejesha fuvu la Mangi Meli kwenda Moshi kaskania mwa Tanzania atapata amani kwa kuwa mwili chifu huyo uliokatwa unahitaji kukamilika.

Bw Mboro ambaye sasa anaishia mjini Berlin anatoka jamii sawa na ile ya Chifu Meeli aliyeuawa na alikuwa akiambiwa hadithi za ujasiri wake.

Nyanya yake alimwambia jinsi alibaki muasi hadi siku ya kifo chake.

Mangi Meli alinyongwa pamoja na watu wengine 18 lakini alichukua muda wa saa saba kufa ishara ya jinsi alikuwa jasiri, Bw Mboro alisema.

Bw Mboro alikuwa ametumia miongo minne kushinikiza mamlaka kufungua makavazi na kuangalia mabaki hayo ya binadamu.

Kwanza ilikuwa ni kupuuza kuliko kakataa ndiyo ilizuia kutafutwa, anasema.

“Kila mtu niliyekuwa nikimuuliza alisema hakufahamu chote kuhusu historia.”

Lakini baadaye aligundua kuwa makavazi ya Charité mjini Berlin yalikuwa na mafuvu na mwaka na 2000 wataalamu wawili waliruhusiwa kuyatazama.

Waligundua kuwa kulikuwa na takriban mafuvu 70 kutoka Tanzania, lakini kulingana na rekodi hakukuwa na vuvu la Mangi Meli.

Kwa Bw Mboro matumaini ni kuwa vuvu la Mangi Meli litarejeshwa, anaendea kusubiri licha ya serikali yake kuonyesha nia ya kurudisha mabaki ya watu.

Lakini Bw Mboro anahisi ni hali nyingine kuchelewa tena na anahofu huenda asitimize ahadi alitoa kwa bibi yake.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *