Home / Uncategorized / Serikali yakamata tani 20 za korosho katika ghala binafsi

Serikali yakamata tani 20 za korosho katika ghala binafsi


Vyombo vya dola nchini Tanzania vimekamata tani 20 za korosho kutoka ghala la Olam linalomilikiwa na mtu binafsi mkoani Mtwara.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema Jumamosi kuwa korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu, limeripoti gazeti la Mtanzania.

“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.

Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje ya nchi au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hicho, Jumanne wiki hii, tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.

Pia imeripotiwa kuwa siku ya Alhamisi iliyopita yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yalioingizwa kutoka Msumbiji.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Gambia akamatwa

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh Maafisa wa polisi nchini Gambia wamemkamata aliyekuwa kiongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *