Michezo

Ole Gunnar Solskjaer apewa kandarasi ya kudumu

Ole Gunnar Solskjaer amekabidhiwa kandarasi ya kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuifunza klabu ya Man United.

Raia huyo wa Norway , 45, aliwasili katika uwanja wa Old Trafford kama kaimu mkufunzi mnmo mwezi Disemba ili kuchukua mahala pake Jose Mourinho.

Solskjaer alihudumu misimu 11 kama mchezaji wa United akifunga goli la ushindi katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya 1999.

“Hii ndio kazi ambayo imekuwa ndoto yangu na sasa nafurahi sana kuweza kuifunza klabu hii kwa muda mrefu”, alisema Solskjaer.

“Kutoka siku ya kwanza nilipowasili, nilijihisi nyumbani katika klabu hii . Ilikuwa heshima kubwa kuichezea klabu hii na baadaye kuanza kazi yangu ya ukufunzi hapa”.

Miezi michache ya kwanza imenipatia tarjiba nzuri sana. Wakati Solskjaer alipochukua usimamizi wa klabu hiyo United ilikuwa ya sita katika ligi ya Premier na pointi 11 nyuma ya viongozi wa nne wa ligi hiyo.

Lakini kufikia sasa wamepoteza mara moja pekee katika klkabu ya Arsenal mwezi huu na sasa wako pointi mbili nyuma ya mbingwa hao wa London ambao kwa sasa wako miongoni mwa klabu nne bora za ligi ya Uingereza.

Solskjaer ndio meneja wa kwanza wa Man United kushinda mechi sita za ligi mfululizo akivunja rekodi iliowekwa na Sir Matt Busby.

United ilifuzu katika michuano ya robo fainli ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 2014 baada ya kubadilisha matokeo ya 2-0 katika mkondo wa kwanza na kuilaza PSG 3-2 nyumbani.

Ushindi huo ulifuatiziwa na ushindi dhidi ya Tottenham, Arsenal na Chelsea huku mfumo wa ushambuliaji katika timu hiyo ukirudishwa.

Na Je Molde?

Solskjaer alikuwa meneja wa klabu ya Molde wakati aliporudi Man United katika makubaliano ya muda

Klabu hiyo ya ya Norway , ambayo msimu wake ulikuwa umekamilika , ilisema kuwa Solskjaer alikubali kandarasi mpya ya miaka mitatu mnamo mwezi Disemba na kwamba walikuwa wanaipatia klabu ya Man United meneja wao.

Hatahivyo habari hiyo imeondolewa katika mtandao wa klabu hiyo na mwezi huu Solskjaer alisema kwamba makubaliano yake na Molde yamepitwa na wakati.

United wanatarajiwa kuilipa Molde mbali na kupanga mechi ya siku zijazo.

Uajiri wa Solskjaer unawacha maswali mengi bila majibu. Hata Ole Gunnar mwenyewe ameshangazwa na kasi aliyokuwa nayo katika klabu hiyo.

Kwa kufanya kile kinachofanyika kiasli amefanikiwa kuwasilisha utulivu katika United baada ya vurugu ilioletwa na Jose Mourinho katika siku zake za mwisho.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close