Habari Za Kitaifa
Trending

Rais Magufuli aipongeza Takukuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 28, 2019 ameipongeza TAKUKURU kwa kufanya kazi nzuri ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini kwa mwaka 2017/18 na kuwataka waongeze makali.

Akiongea kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa ripoti ya TAKUKURU na kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, amewaonya pia TAKUKURU kutowaonea watu katika utendaji wao na kuwataka wafanye kazi kwa bidii.

Katika ripoti hiyo iliyosomwa na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Kamishna Diwani Athuman, imeeleza kuwa Katika kipindi cha mwaka 2017/18 TAKUKURU imefanikiwa katika utendaji wake wa kazi kwa 81.4% na kuweza kuokoa kiasi cha TSh Bilioni 70.3 katika mwaka huo.”.

Tags
Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close