Michezo
Trending

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 01.04.2019

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hatma ya mshambuliaji wa Wales Gareth Bell ,29, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Man Unted mbali na kurudi Tottenham, utaamuliwa mwisho wa msimu huu.(Talksport)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anafikiria kuwasilisha dau la £35m ili kumnunua beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21. (Mail)

Barcelona imewasiliana na babake Juan Mata na ajenti Juan Sr kuhusu uwezekano wa kiungo huyo wa Manchester United, 30 na Uhispania ambae kandarasi yake imekwisha kuhamia katika klabu hiyo.. (Sun)

Hatma ya siku zijazo ya Jan Siewert kama mkufunzi wa Huddersfield haijulikani baada ya kushushwa daraja katika ligi ya Uingereza kutokana na kuvunjika kwa uhusiano wake na wachezaji wapya wa klabu hiyo. (times)

Manchester United inakataa kukubali mahitaji ya mshahara wa Ander Herrera wa £200,000 kwa wiki licha ya kandarasi ya kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 29 kukamilika mwisho wa msimu huu mbali na kufuatiliwa na PSG . (Mirror)

Leicester inafikiria kuwasilisha dau la £40m ili kuimarisha mkopo wa kiungo wa kati wa Monaco na Ubelgiji Youri Tielemans, 21, kuwa uhamisho wa kudumu. (Mail)

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anatumai klabu hiyo itachukua fursa nzuri iliopo kumsaini mchezaji wa Barcelona na Ureno aliyepo kwa mkopo Andre Gomes, 25, ambaye pia analengwa na Inter Milan, kwa mkataba wa kudumu. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa zamani wa klabu ya West Ham Harry Redknapp angependelea kumuona kiungo wakati wa Uingereza na nahodha Mark Noble, 31, kuifunza klabu hiyo siku moja baada ya kumaliza kucheza soka. (Star)

David Beckham anasema kuwa mchezaji mwenza wa zamani Ole Gunnar Solskjaer anahitaji kuwa mkufunzi mpya wa Manchester United kutokana na kazi nzuri aliofanya wakati alipokuwa kaimu mkufunzi . (Manchester Evening News)

Arsenal inafikiria kumpatia mshambuliaji wake anayeuguza jeraha Danny Welbeck kandarasi mpya huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akitarajiwa kuanza kufanya mazoezi kabla ya msimu huu kuisha. (Independent)

Beki wa Everton na jamhuri ya Ireland Seamus Coleman, 30, anataka klabu hiyo kutumia fedha nyingi mwisho wa msimu huu iwapo itarudi kucheza katika kombe la Ulaya. (Independent)

Darren Moore amekiri alishangazwa alipotolewa nje kama mkufunzi wa West Brom . (Express and Star)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa timu yake inahitaji kucheza mechi zake zote zilizosalia kama mashine iwapo inataka kushinda mataji manne msimu huu . (telegraph)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri anasisitiza kuwa amezoea wito wa mashabiki wanaotaka afutwe kazi (Express)

Kiungo wa zamani wa Inter na Manchester United Juan Sebastian Veron, aliyeshiriki katika ufunguzi wa uwanja mpya wa Tottenham wikendi iliopita , anaamini Spurs itaweza kuvutia wachezaji wengi wa kiwango cha juu kutokana na nyumba yao mpya.. (Mirror)

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Back to top button
Close