Habari Za Kitaifa
Trending

JPM awaweka kikaangoni wakurugenzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya Wakurugenzi ambao wataonyesha nia ya kudai ushuru kufuatia uamuzi wa Serikali, kununua zao la Korosho kwa bei elekezi ya shilingi 3300, baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya wakulima na wafanyabiashara wa Korosho.

Ametoa onyo hilo akiwa ziarani mkoani Mtwara wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Mtwara kuelekea Newala na Masasi, ambapo amesema serikali haiwezi kuamua kuwasaidia wananchi halafu Halmashauri ijitokeze kutaka ushuru.

”Halmashauri mmeshindwa kusimamia korosho, baada ya kupewa bei nzuri wanapewa 1500, tukasema hapana tukakopa ili tuwalipe, nione Mkurugenzi ananiomba hizo hela, aone kama ataendelea kuwa Mkurugenzi, utaombea kijijini ukiwa unalima,”

Aidha, amesema kuwa haiwezekani serikali ipange kununua Korosho kwa bei ya 3300 halafu ianze kulipia kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho, hivyo amesema kama wanataka ushuru wasimamie vizuri bei ya korosho.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameanza ziara ya kikazi Mkoani Mtwara ambapo ameanza April 2, 2019. Amefanya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi kwenye viwanda cha kubangua korosho cha Yalin pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close