Habari za Kimataifa
Trending

Adaiwa kumuua mkewe siku chache baada ya ndoa

Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumuua mkewe mjamzito aliyefunga naye ndoa siku chache zilizopita.

George Marito mwenye umri wa miaka 28 anadaiwa kutenda kosa hilo Jumapili iliyopita ambapo alimpiga Dorcas Nyaboke hadi kufa kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi na mashuhuda baada ya kutekeleza tukio hilo alijaribu kujiua kwa kujirusha kwenye maporomoko ya mto Kegati lakini kuna mpita njia aliyemuona baadaye akamuokoa na kumrudisha nyumbani kwake.

“Baada ya kumfikisha nyumbani, yule jirani yetu alishtuka kuona mwili wa Nyaboke ukiwa umelala sakafuni, pembeni kuna matapishi,” jirani aliyejitambulisha kwa jina la Isaboke alizungumzia tukio hilo.

Uchunguzi wa awali wa polisi umeeleza kuwa Marito alirejea nyumbani kwake Jumapili usiku majira ya saa nne, na alipoulizwa na mkewe sababu za kurejea usiku huo kwani amechelewa walitofautiana kauli na ndipo alipoanza kumpiga.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close