Home / Ujasiriamali / JIFUNZE KUPIKA SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

JIFUNZE KUPIKA SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

Vipimo

 

 

Kuku                                                            4 LB

 

Viazi/mbatata                                              3

 

Kitunguu maji                                               1

 

Kitunguu saumu(thomu/galic)                       5 chembe

 

Pilipili mbichi                                                  2

 

Nyanya ya kusaga                                       1 kijiko cha chai

 

Pilipili manga ya unga                                    ½  kijiko cha chai

 

Haldi/tumeric/bizari ya manjano                    ¼  kijiko cha chai

 

Mafuta ya zaytuni                                         2 vijiko vya supu

 

Kotmiri (coriander freshi)                              1 msongo

 

Ndimu/siki                                                    2 vijiko vya supu

 

Chumvi                                                        kiasi

 

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 

 

  1. Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi

 

 

  1. Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.

 

 

  1. Menya kitunguu maji ukate vidogodogo

 

 

  1. Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.

 

 

  1. Kisha  tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.   

 

  1. Tia nyanya,  haldi, na maji kiasi.

 

 

  1. Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.

 

 

  1. Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.

 

 

  1. Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa  na mkate au upendavyo

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Zao la muhogo linavyoweza kupaisha uchumi wa wakulima

TANZANIA ina fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa muhogo hata kuongoza katika Afrika kutokana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *