Home / Habari za Kimataifa / MSICHANA ALIYETENGWA KWA KUWA NA HEDHI AFARIKI.

MSICHANA ALIYETENGWA KWA KUWA NA HEDHI AFARIKI.

Jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa

Maafisa wa polisi huko Nepal wanachunguza kifo cha msichana wa miaka 15 aliyefukuzwa hadi katika mtaa wa mabanda kwa kutokwa na hedhi.

Wanasema kuwa msichana huyo alikosa hewa na kufariki baada ya kuwasha moto ili kupata joto.

Chini ya tamaduni za Hindu kwa jina Chhaupadi, wanawake walio na hedhi ama ambao wamejifungua huonekana kuwa wachafu.

Tamaduni hiyo ilipigwa marufuku na serikali ya Napoli mwaka 2005, lakini bado inaendelea kutekelezwa katika maeneo ya mashambani yaliopo magharibi.

Mwili wa Roshani Tiruwa ulipatikana na babake wikendi iliopita katika jiwe na nyumba moja ya matope katika kijiji cha Gajra, Wilayani Accham yapata kilomita 440 magharibi mwa Kathmandu.

Baadhi ya jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa.

Huku wakiwa wametengwa hunyimwa chakula chao cha kila siku na hawaruhusiwi kunywa maziwa.

source bbc swahili.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *