Home / Habari za Kimataifa / MKOSOAJI WA CHINA ATEULIWA KUONGOZA BUDI YA BIASHARA US.

MKOSOAJI WA CHINA ATEULIWA KUONGOZA BUDI YA BIASHARA US.

Rais mteule Donald Trump amemteua mkoasoaji mkubwa wa taifa la China kuwa kiongozi wa bodi ya biashara

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, amemtaja mkosoaji mkubwa wa biashara za Kichina Peter Navarro kuwa kiongozi mkuu wa baraza jipya la kibiashara katika Ikulu ya White House.

Peter Navarro, alizindua sera ngumu dhidi ya Beijing na akaandika kitabu kwa jina “Death by China: How America Lost its Manufacturing Base”. Yani kifo cha China: namna Marekani ilipopoteza uwezo wake wa uundaji bidhaa”

Serikali ya mpito ya Doland Trump, imemsifu kwa uwezo wake wa kufufua uchumi, mbali na kukabiliana na uhaba wa kazi kwa Wamarekani.

Peter Navarro mkoasoaji mkubwa wa China

Bwana Trump pia, ameteua mwekezaji bilionea na msomi wa uchumi, Carl Icahn, kama mshauri mkuu wa mageuzi.

Bw Icahn, amesema kuwa biashara nchini Marekani, imelemazwa na masharti mengi yasio na maana.

SORCE BBC SWAHILI

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *