Home / Habari za Kimataifa / SERIKALI NA UPINZANI WAAFIKIA MWAFAKA DR CONGO.

SERIKALI NA UPINZANI WAAFIKIA MWAFAKA DR CONGO.

Miongoni mwa mashari ya mwafaka huo ni rais Kabila kutogombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018

Wapatanishi wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka makundi ya upinzani sasa wameafikia mwafaka.

Maaskofu kutoka kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 12.

Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo.

Mda wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong’atuka kwake kumesababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 40 wamefariki.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *