Home / Habari za Kimataifa / ZAIDI YA MABOMU 9000 YAMETEGULIWA IRAQ NA SYRIA.

ZAIDI YA MABOMU 9000 YAMETEGULIWA IRAQ NA SYRIA.

Shirika la The Mines Advisory Group, linasema limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita

Shirika linalopinga matumizi ya mabomu yanatotegwa ardhini, limesema kuwa fedha zaidi zinahitajika kupambana na tatizo linalozidi nchini Syria na Iraq.

Shirika hilo, The Mines Advisory Group, linasema limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita, katika maeneo ambayo yalikuwa yamedhibitiwa na Islamic State.

Linasema zinahitajika dola milioni 100 zaidi, kutegua mabomu yaliyotegwa karibuni, na maelfu mengine yaliyobaki kutoka na vita vya zamani.

Wito huo wa mchango, umetolewa ikiwa imetimia miaka 20 kamili, tangu Hayati Princess Diana kuzuru maeneo yaliyozikwa mabomu huko Angola ziara iliyosaidia kuzindua ulimwengu kuhusu tatizo hilo.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *