Home / Habari Za Kitaifa / KIJAJI: TUMIENI USOMI KWA MAENDELEO YA NCHI.

KIJAJI: TUMIENI USOMI KWA MAENDELEO YA NCHI.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amewataka wasomi wanaohitimu masomo mbalimbali ngazi ya shahada na astashahada kuhakikisha wanautumia vyema usomi wao kwa manufaa ya nchi.

Dk Kijaji aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mahafali ya wahitimu zaidi ya 171 wa Shahada ya Pili katika fani mbalimbali ikiwemo manunuzi, ugani na uhasibu.

Alisema, baadhi ya wasomi wamekuwa wakitumia kalamu zao vibaya na kuisababishia serikali hasara kwa kujijali wenyewe badala ya maslahi ya taifa.

Alisema anategemea wasomi watasimamia sheria na taratibu za kazi ili kuleta tija kwani awamu hii ni ya kuleta maendeleo kwa jamii kwa kuwatumia wasomi katika nyanja mbalimbali ili kuleta manufaa.

“Lazima sasa wasomi watumie kalamu zao kwa uaminifu badala ya kujinufaisha, lakini pia napongeza uongozi wa chuo hiki kwa kuhakikisha inatolewa elimu bora kwa kushirikiana na wenzetu wa chuo kikuu cha Coventry cha Uingereza,” alieleza Dk Kijaji.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro (IAA), Dk Faraji Kasidi, alisema chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali kwa kushirikiana na Chuo cha Coventry cha Uingereza, lengo ni kuhakikisha taifa linakuwa na wasomi katika sekta mbalimbali ikiwemo kuwafundisha ujasiriamali.

Alisema baadhi ya wasomi wanafikiri ukisoma tu unapata ajira bila kujua pia kuwa kuna fursa za kujiajiri wenyewe mara wamalizapo vyuo.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqro, alitoa rai kwa wasomi hao kuhakikisha wanaopenda kufanya kazi wanasimamia haki kwa kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwa na uzalendo kwa nchi yao na kuepuka rushwa ambayo ni adui wa haki.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *