Home / Michezo / Claudio Ranieri: Meneja wa Leicester anataka Antonio Conte ashinde EPL

Claudio Ranieri: Meneja wa Leicester anataka Antonio Conte ashinde EPL

Ranieri ndiye Mwitaliano wa tatu kushinda EPL baada ya Carlo Ancelotti (Chelsea mwaka 2009-10) na Roberto Mancini (Manchester City mwaka 2011-12)

Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri amesema anataka sana Mwitaliano mwenzake Antonio Conte ashinde Ligi ya Premia na viongozi wa ligi wa sasa Chelsea.

Ranieri, 65, aliongoza Leicester kushinda ligi msimu uliopita kwa njia ya kushangaza.

Lakini kwa sasa Leicester wamo nambari 15 ligini, alama 34 nyuma ya klabu hiyo yake ya zamani.

“Kama mkufunzi wa zamani wa Chelsea na shabiki wa Italia, natumai Conte atatimiza lengo hilo,” Ranieri amesema.

“Ameonesha kwamba makocha wa Italia ni stadi sana.”

Ranieri ana mkataba Leicester hadi 2020 lakini anakubali kwamba nafasi yake katika klabu hiyo haiko salama, licha ya kufikia ufanisi wa kushangaza msimu uliopita.

“Natumai nitasalia England,” aliongeza.

“Ninahisi vyema hapa, ingawa katika kandanda mnakuwa juu kwenye nyota leo na kesho yake mnajipata chini sakafuni, kwa hivyo usiwahi kudhania umefika.”

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *