Home / Imani / NAMNA YA KUKOSOANA KATI YA WALINGANIAJI (MADUATI) NA JINSI YA KUREKEBISHANA

NAMNA YA KUKOSOANA KATI YA WALINGANIAJI (MADUATI) NA JINSI YA KUREKEBISHANA

الجزء السابع

Juzuu ya saba

مجموع فتاوي ومقالات متنوعة

من صفحة : 316- 321

Maj-muu fataawa wamaqaalaati mutawiatu

Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe , na rehma na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad , Nabii aliye mwaminifu , pia amani ziwafikie Ahli zake na mas-haba zake , Na kila anayefuata na kutekeleza Sunna zake mpaka siku ya Qiyama.

Ama baada ya utangulizi huo : hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha watu kuwa waadilifu na wenye kufanya wema , Na anakataza dhulma , kuchupa mipaka , na uadui . Mwenyezi Mungu amemtuma Mtume wake Muhammad kwa kilekile alichowatuma Mitume wote : katika kuwaita watu kwenye Tauhidi na kutakasa ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mmoja

alimuamrisha kufanya uadilifu , Na akamzuia kufanya kinyume na hayo khasa katika kuabudu kinyume na Mwenyezi Mungu mmoja , Na akamzuia kufarikiana na kutengana na kufanyiana uadui dhidi ya haki mbalimbali za waja.

Hakika watu wengi wanaojinasibisha na elimu na kuita watu katika mambo ya kheri (daawa) imeenea sana katika zama hizi wengi wao wanajitumbukiza katika shimo la kuvunja heshima za ndugu zao mashuhuri wanaojishughulisha na kazi kubwa ya kuita na kufahamisha watu katika mambo mbalimbali ya kheri , huku wakitafuta pia kuharibu heshima za wanafuzi , walinganiaji , na wahadhiri mbalimbali . na hufanya kazi hiyo ya kuchokonoa hali za watu katika vikao vyao vya siri , na huwenda wengine wakarekodi katika kaseti na kuenezwa kwa watu , bali wengine hufanya hayo katika mihadhara ya wazi katika misikiti , Hakuna cha maana kinachongumzwa zaidi ya kutajwa Fulani na Fulani wanafanya kadhaa au wana kadhaa .

Kwani utaratibu huu ni kinyume kabisa na maamrisho ya Mwenyezi Mungu juu ya Mitume wake kwa vigezo vingi miongoni mwa sababu hizo ni :

  1. Kazi hii ya kufuatilia heshima za watu huhesabiwa ni kuporomosha haki za watu katika waislamu , hususani wanafunzi na walinganiaji ambao wametoa juhudi zao kubwa katika kuwafahamisha watu na kuwapatia mwongozo , na kusafisha itikadi zao na mwelekeo wao , wamejitahidi kupangilia masomo na mihadhara mbalimbali , pia kutunga vitabu mbalimbali vyenye manufaa.

  1. Kitendo hicho ni kufariqisha umoja wa Waislamu na kutenganisha mshikamano wao , ukizingatia kuwa hivi leo Waislamu wana haja kubwa ya kuwa kitu kimoja na kujiepusha na mitawanyiko na makundi , pia kutokuwa na muda wa porojo baina yao , hususani hao madai ambao wanachafuliwa miongoni mwao ni katika watu wanaoshikamana na Sunna za Mtume Muhammad na kuwa pamoja na watu (ahli Sunna wal-jamaa) wanaojulikana kwa kupambana na uzushi na mambo yasiyo na mashiko katika dini , na kumhadharisha yule anayeita watu katika mazushi , pia kufichua mikakati na michezo yao ambayo lengo lake ni kuwashughulisha Waislamu wasiwe na muda wa kufuata na kutekeleza dini yao . Na ukweli wa mambo hatuoni faida yoyote katika kazi hii ya kuchokonoachokonoa mambo na hali za watu , ila sana Wanafiqi , Makafiri , waovu , na wazushi katika dini ndiyo watakaofaidika kwa kufurahi watakavyoona waislamu wanarumbana wao kwa wao .

  1. Vitendo wanavyovifanya watu hawa kuna ishara kubwa kabisa ya kuwasaidia wamagharibi na secularism1 na wengineo kama makomunist2 ambao wanajulikana kwa uongo na uadui mkubwa dhidi ya walinganiaji wa dini ya MwenyezuMungu , na kuwahamasisha watu wafuate yale waliyoyaandika na kuyarekodi . Hivyo basi si haki kabisa ya udugu wa Kiislamu kuwasaidia watu kama hawa ambao pupa yao ni dunia , kwani hawa ni maadui dhidi ya ndugu zao Wanafunzi wa sheria ya Allah na walinganiaji wa dini ya Allah (madaai) .

  1. Vitendo hivyo ni kuharibu nyoyo za waislamu wengi wasiojua dini yao kwa undani , pia ni kuwachanganya na kuwashughulisha wanachuoni wetu , pia hali hiyo ni kueneza na kupambia uongo na vitu visivyo sahihi , ni sababu ya kuzidi utesi na usengenyaji , ni ufunguo wa shari dhidi ya waenezaji wa machafuzi hayo kwa udhaifu wa nafsi zao , na ni uchochezi wa fitina , na wanapupia kuwaudhi waumini pasina makosa yoyote waliyoyafanya .

  1. Utakuta maneno mengi yaliyosemwa hayana uhakika , ispokuwa ni tuhuma alizowadanganya na kuwapambia sheitwani , anasema Mwenyezi Mingu mtukufu :

3 يَأيُّهَا الّذِ يْنَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كًثِيْرًا مِنَ الظَّنِِ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ , وَلًا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَبْ بَعَضُكُمْ يَعْضَا

Enyi mlionamini ! jiepusheni sana na (kuwadhania watu) dhana (mbaya) kwani (kuwadhania watu ) dhana (mbaya) baadhi ya dhana ni dhambi . wala msipeleleze (habari za watu). Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine … 4 .

Na muumini wa kweli anatakiwa amdhanie vizuri mwislamu mwenzake katika maneno yake . wamesema baadhi ya Masalafu :[ usilidhanie vibaya neno linalotoka katika kinywa cha nduguyo , hali ya kuwa neno hilo unaliona kabisa kuwa lina nafasi katika kheri ] .

  1. Katika jambo lolote ambalo linawezekana mtu kutoa jitihada zake za ufahamu katika mambo ya sheria kwa baadhi ya wanachuoni au Wanafunzi waliofikia kujitahidi , mwenye jitihada hizo halaumiwi wala haonekani kuwa kafanya makosa kwa sharti kama atakuwa mtu huyo ni katika wale ambao wanaruhusiwa kujitahidi (iwapo watatimiza masharti ya kuwa mujitahidu) , Hivyo basi iwapo mwingine atampinga kauli yake katika mambo kama haya ya jitihadi basi atumie maneno mazuri na wala si matusi na kufedheheshana , na awe na nia ya kufahamishana ukweli ni upi unaofaa kufuatwa , kauli nzuri pia inakuwa ni sababu ya kuzuia wasiwasi wa shaitwani na vichochezi vyake baina ya waumini , na iwapo hatoweza kutumia maneno mazuri na akaona kuna haja ya kubainisha kosa alilolifanya au kulisema ndugu yetu basi atumie sentesi nzuri na ibara zisizo na hamasa ndani yake .

Na maelekezo ya upole bila kushambuliana au kutiana dosari au kutoleana maneno machafu ambayo yatampelekea hata yule mlengwa wa maneno hayo kupuuzia haqi na ukweli pengi kutokuufata kabisa . Na isiwe kwa kutaja majina ya watu walengwa au kutuhumiana nia za watu (amesema au amefanya kadha kwa sababu ana kusudia kadha) , Au pia kuzidisha maneno ambayo hayana sababu ya kuongezwa . Kwani Mtume wetu Muhammad alikuwa akisema katika mfano wa mambo kama haya : {{ ما بال أقوام قالوا كذا وكذا }}

(( Kulikoni basi watu wanasema Kadha na Kadha )) ( hakutaja jina la Mtu wala jina sehemu Kijiji ).

Hivyo basi kitu muhimu ninachowahusia hawa ndugu zangu ambao tayari wamejiingiza katika shimo la kuwachafua na kuwatia dosari walinganiaji wa dini ya Allah (Madaai) watubie kwa MwenyeziMungu juu ya yale waliyoyaandika au kuyasema kwa kuwashambulia ndugu zao , hali ambayo imekuwa ni sababu kubwa ya baadhi ya vijana kuharibika na kujaa chuki na vifundo katika nyoyo zao , Bali wamejishughulisha na mambo hayo kushambuliana na wameacha kutafuta elimu yenye manufaa katika Dini na Dunia yao . Pia wameacha kuwaita watu katika Kheri na wamekalia Porojo na kuwazunguzia Fulani kadha Fulani kadha , huku wakitafuta na kuwinda kwa wenzao kila wanachokiona , Hili ni kosa kwao . Wao wanatafuta makosa japo hata kwa kulazimishia ili mradi waonekane wenzao wana makosa na wao wako sahihi .

Huku nikiendelea kuwanasihi wasafishe na kuoandoa haya waliyokwisha kuyasema au kuyaandika , Waseme tena au waandike mara nyingine maneno mengine ambayo yanarekebisha makosa yao ya kuwatuhumu wenzao mambo yaliyo mbali nao , na waondoe ufahamu uliojengeka kwa watu kupitia maneno yao mabaya waliyoeneza , na wajishughulishe na mambo ya kheri yanayowakurubisha kwa mwenyezimungu na kuleta manufaa katika uislamu na waislamu , na wajihadhari sana na kukimbilia kuwakufurisha au kuwahukumu wenzao waovu au wazushi pasi na dalili wala ushahidi unaoonyesha kuwa watu hawa wana sifa hizi , amesema Mtume Muhammad 

{{ من قال لأخيه يا كافر , فقد باء بها أحدهما}} متفق على صحته

((Yeyote mwenyekusema kumwambia ndugu yake : Ewe Kafiri ; basi neno hilo tayari limemuhusu mmoja wao )) , (kama muambiwaji hana huo ukafiri , ukafiri utakuwa ni wa msemaji ) .

Katika utaratibu ulio wa sawa inatakiwa kwa walinganiaji na wanafunzi wanapopata tatizo lolote katika maneno ya wanachuoni au wengineo , warejee kwa wanachuoni wanaotegemewa na jamii wawaulize ili wawasaidie na kuwaondolea shubuha na shaka katika sehemu zilizo watatiza na wawabainishie ukweli unaokusudiwa katika maneno hayo , yote haya ni kufanyia kazi kauli ya mwenyezimungu pale aliposema :

وإذا جآءهم أمرمن الأمن أو الخوف أذاعوا به ج ولو ردّه إلى الرسول وإلى أولى الأمرمنهم لعلمه الّذين يسنبطونه منهم ق ولولا فضل الله عليكم ورحمته لا تبعتم الشيطان إلاّقليلاً83 5

Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza . na kama wangalilipeleka kwa mtume na kwa wenye mamlaka kwao , wale wanaopeleleza (wanaojua kupima mambo) miongoni mwao wangalijua (kuwa hilo ni jambo la kutangazwa au si la kutangazwa ). Na kama isingalikuwa fadhila ya Mwenyezi Mungu juu ya (wengi katika) nyinyi na rehema yake, kwa yakini mngalimfuata shetani ispokuwa wachache au (waliopata fadhila hiyo 6

Kwani kutengemaa hali za waislamu wote kwa ujumla , nyoyo zao kuwa kitu kimoja , kuwa na matendo ya uchamungu , kuwezekana wanachuoni wote wa kiislamu na walinganiaji wa kila kinachomridhisha mwenyezimungu na kuwanufaisha waja wake kuwa katika msimamo na mwongozo , kuwa neno lao ni moja katika uongofu , kukingwa na sababu za kukhitilafiana na kutofautiana , kupata nusura katika dini na kuondoka mambo batili kupitia sisi , ni jambo linalomuhusu Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye msimamizi na mwenye uwezo juu ya hayo.

Rahma na amani zimfikie mtume wetu Muhammad na ahli zake na mas-haba zake na kila atakayeongoka kwa mwongozo wake mpaka siku ya malipo (qiyama).

Swali la kwanza : Katika mawiki yaliyopita mlibainisha utaratibu na njia za kukosoana kwa walinganiaji , baadhi ya watu walitafsiri maelekezo hayo katika njia tofautitofauti , ninyi mnatusaidiaje katika hilo ? muulizaji : A , F, A .

Jawabu : Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu , na Rehema na Amani zimfikie Mtume wa allah na kila atakayeongoka kwa mwongozo wake .

Ubainifu huu aliyokusudia muulizaji tulikusudia kutoa nasaha kwa ndugu zetu wanachuoni na walinganiaji kuwa inatakiwa ukosoaji wao kwa ndugu zao kupitia maneno , mikutano au mihadhara mbalimbali uwe ni urekebishanaji wa kujenga usio na kuchafuana na kutaja majina ya watu , kwa sababu hali hii inaweza kusababisha , vifundo vya chuki na uadui kati yao wote .

Ilikuwa kawida na taratibu zake Mtume Muhammad anapofikiwa na jambo lolote linalokwenda kinyume na sheria kati ya mas-haba zake , Huhadharisha jambo hilo kwa kusema :}} ما بال أقوام قالوا كذا وكذا {{

(( kilikoni watu wanasema kadha na kadhaa)) kisha Mtume anabainisha huo uovu uliofanyika nini hukumu yake kwa mujibu wa Sheria .

Mfano wa utaratibu wake huo ; Ilimfikia habari kuwa baadhi ya watu wamesema : “Ama mimi nitakuwa ni mwenye kuswali kila siku (Qiyamu llayli) wala sitaki kulala” mwingine Akasema : “ Mimi nitafunga siku zote wala sitaki kula mchana” na mwingine Akasema : “Ama mimi sitaki kuoa wanawake” Mtume baada kumfikia taarifa hizo , aliwahutubia watu , akasifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu na Akasema :

{{ما بال أقوام يقولون كذا وكذا , لكني أصلي وأنام , وأصوم وأفطر, وأتزوّج النّساء , فمن رغب عن سنّتي فليس منّي }}

(( Inakuwaje watu wanasema Kadha na Kadha : Mimi mwenyewe ninaswali usiku na ninalala (Sikeshi nikifanya ibada) , ninafunga na ninakula (Ninafunga baadhi siku sio siku zote ) , na ninaoa wanawake , yeyote mwenye kuchukia Sunna zangu basi si katika mimi ( Si katika watu wanaofuata mwongozo wangu ), )) .

Kusudio langu ni haya maneno ya Mtume Muhammad aliyosema kuwa ; mtu anapowahadharisha watu anatakiwa atumie mfano wa maneno kama haya kwa kusema :

baadhi ya watu wamesema au wanasema Kadhaa , na Sheria ya jambo hilo ni Kadhaa , na ulazima wa kutekeleza katika jambo hilo ni Kadhaa” , maana yake unakosoa na kurekebisha pasi na kutaja Mtu Maalumu , ispokuwa lililo la muhimu hapo wewe unataka kubainisha jambo hilo kwa mujibu wa Sheria . Na tukienda na utaratibu huu , mapenzi na kuhurumiana vitaendelea kuwapo baina ya wanachuoni , walinganiaji , na ndugu wote wa Kiislamu kwa ujumla.

Mimi kusema hivi sikusudii nasaha hizi watu Fulani tu , bali ninakusudia wanachuoni na wanaharakati wote ndani na nje ya nchi ( ya Saudi Arabia) .

Hivyo basi hasaha zangu ninasema : Majadiliano yanayohusu kunasihiana na kuwekana sawa yawe kwa njia ya kuficha jina au Sehemu kwani lengo kuu ni kuhadharisha na kuzindua watu juu ya kosa lililofanyika , na ukweli kuhusu Sheria juu ya jambo hilo , bila kuleta mambo ya kuchafuana Fulani na Fulani .

Mwenyezi Mungu atuwezeshe wote tuwe katika usawa.

Imetolewa na ;

Fadhwilatu shekh ; Abdul-azizi bin Abdullah bin Baazi

Aliyekuwa ; Mkurugenzi Mkuu wa Idara mbalimbali za pekuzi za Kielimu

Fat-wa , Daawa na mingozo mbalimbali .

Pia aliwahi kuwa: Mufti wa Saudi Arabia.

Imefasiriwa na;

Amry Ally Shambula.

Trh; 29/6/2010 m & mwezi 17/ Rajabu / 1431.

Temeke – Dar-es-salaam.

0714- 839860.

Ni kundi linalohamasisha watu wajishughulishe na watenganishe kati ya dini na dunia . na harakati zilianzia katika bara la ulay الدال

Tafsiri ya shekhe : Abdullah Al-faarisiy .4 سورة الحجرات 49/ الآية 12a .(الموسوعة الميسرة في الأديان والمذاهب والفرق المعاصرة ص 679 Ni watu wasiomuamini mungu na wanafanya dhuluma na mafisadi mbalimbali “ لسان العرب , حرف سورة النّساء 4 / الآية 8 Tafsiri ya shekhe : Abdullah Al-faarisiy . 3

1 Ni kundi linalohamasisha watu wajishughulishe na watenganishe kati ya dini na dunia . na harakati zilianzia katika bara la ulaya .(الموسوعة الميسرة في الأديان والمذاهب والفرق المعاصرة ص 679)

2 Ni watu wasiomuamini mungu na wanafanya dhuluma na mafisadi mbalimbali لسان العرب , حرف الدال

34 سورة الحجرات 49/ الآية 12 .

4 Tafsiri ya shekhe : Abdullah Al-faarisiy .

5 سورة النّساء 4 / الآية 83 .

6 Tafsiri ya shekhe : Abdullah Al-faarisiy .

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mwanasaikolojia achambua sababu za mtu kujitoa uhai

KIFO cha mwanasayansi kikongwe wa Australia, David Goodall (104) aliyetimiza azma yake ya kujiua kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *