Home / Michezo / Ian Wright: Wenger aliniambia muda wake unakaribia kikomo Arsenal

Ian Wright: Wenger aliniambia muda wake unakaribia kikomo Arsenal

Wenger amenukuliwa akisema kuwa huenda akaondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu

Arsene Wenger amemwambia Ian Wright kwamba muda wake kama mkufunzi wa Arsenla unakaribia kikomo kulingana na mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal.

Wenger ameifunza Arsenal tangu mwezi Oktoba 1996 na mara ya mwisho yeye kushinda taji la ligi ilikuwa mwaka 2004.

Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu huu.

”Ninahisi kwamba ameamua”, mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal aliambia BBC Radio 5 live.

”Anaonekana amechoka.Unahisi kwamba anaonyesha uchovu.Nadhani atawachia mwishoni mwa msimu huu”.

Matumaini ya Arsenal ya kushinda taji la ligi msimu huu yalipata pigo kubwa baada ya kushindwa 3-1 na viongozi wa ligi Chelsea kuwawacha wakiwa pointi 12 nyuma ya Chelsea.

Wright anasema kuwa aliongea na Wenger usiku wa Alhamisi.

”Aliniambia kwamba anafikia kikomo.Sijamsikia akisema hivyo awali”,alisema Ian Wright mwenye umri wa miaka 53.

”Wachezaji wamemuangusha sana.Iwapo hataondoka mwisho wa msimu huu kutakuwa na mabadiliko makubwa mwishoni mwa msimu huu.Wanafaa kujiangalia sana.Amekuwa mwaminifu kwa timu hii”.

Baadhi ya mashabiki wamemtaka Wenger kuondoka ,huku mmoja akibeba bango katika uwanja wa Stamford Bridge lililosema ”Imetosha! Ni wakati unafaa kuondoka”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *