Habari za KimataifaSlider

MAANDAMANO YA ‘UMOJA’ MEXICO KUMPINGA DONALD TRUMP.

Waandamanaji wamewataka raia wa Mexico kuungana dhidi ya Trump

Maelfu ya watu wameandamana nchini Mexico kupinga sera za uhamiaji za rais wa Marekani Donald Trump pamoja na mpango wake wa kujenga ukuta katika mpaka wa mataifa hayo mawili.

Waandamanaji katika zaidi ya miji kumi Mexico, waliandamana barabarani wakiwa wamevalia mavazi meupe na kupeperusha bendera za Mexico na kubeba mabango ya kumshutumu Trump.

Waandalizi wanasema walitaka kutuma ujumbe kwamba Mexico imeungana dhidi ya Trump.

Pia walimshutumu Rais Enrique Pena Nieto kwa kutokabiliana vilivyo na rushwa na ongezeko la uhalifu wa kutumia mabavu.

Mmoja wa waandamanaji Maria Amparo Cassar amesema sera za uhamiaji za Trump ni “tishio kwa jamii ya kimataifa.”

“Isisahaulike kwamba jamii ya Marekani iliundwa na wahamiaji na inaendelea kuundwa na wahamiaji,” amesema.

Raia wa Mexico wanatazama sera za uhamiaji za Trump kuwa zisizo za haki

Waandamanji katika mji mkuu, Jiji la Mexico, walibeba mabango ya kuonyesha umoja.

Moja lilikuwa na ujumbe: “Gracias, (Asante) Trump, kwa kuunganisha Mexico!”

Bw Trump anapanga kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico na amekuwa akisisitiza kwamba raia wa Mexico ndio watalipia ujenzi huo.

Hilo limewakera taia wa Mexico na rais Pena Nieto mara kwa mara amesisitiza kwamba taifa lake halitalipia ukuta huo.

Majuzi, mkutano uliopangwa kati ya wawili hao ulitibuka.

Maelfu ya watu waliandamana Mexico City, na hapa wanaonekana Plaza Angel Independencia

Waandamanji wamesema wanataka kuonesha wameungana dhidi ya Trump

SOURCE BBC SWAHILI.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close