Home / Habari za Kimataifa / Wapata mlo na kisha kutimka mbio kutoka hotelini bila kulipa

Wapata mlo na kisha kutimka mbio kutoka hotelini bila kulipa

Watu hao walitimka mbio kutoka mgahawa wa El Carmen

Takriban watu 120 waliokuwa wakipata maankuli kwenye mgahawa mmoja kaskazini magharibi mwa Uhispania, walikimbia wote kwa pamoja na kukosa kulipa.

Watu hao raia wa Romania ambao walikuwa mwanzo wamelipa euro 900, waliondoa kwenye mgahawa wa El Carmen wati walikaribia kupata mlo wa keki.

“Ilitokea kwa dakia moja tu, ni kitu walikuwa wamepanga kwa sababu walitoka kwa kutimka mbio.” alisema mmiliki wa hoteli Antonio Rodriguez .

Sasa wana deni la euro 2,000 kwenye hoteli hiyo.

Watu hao walikuwa wamepata chakula cha kwanza, chakula kikuu, na chupa 30 za mvinyo, na Rodriguez anasema kuwa hiyo ndiyo mara ya kwanza ndani ya miaka 35 amefanya kazi ya hoteli kushuhudia kisa kama hicho.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *