Home / Habari Za Kitaifa / Shule zitakazokiuka mihula miwili kukiona

Shule zitakazokiuka mihula miwili kukiona

MAKATIBU tawala na wakurugenzi wa halmashauri ambao ndio wasimamizi wa shule zote nchini, wametakiwa kuzichukulia hatua shule zote zitakazokiuka utekelezaji wa Mwongozo wa mihula miwili tu kwa mwaka.

Mwongozo huo uliotolewa mwaka jana na Serikali kwa ajili ya kuanza kutekelezwa mwaka huu, uko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Baada ya kutolewa kwa waraka huo namba moja wa mwaka 2015, unapiga marufuku shule kuwa na mihula zaidi ya miwili.

Akizungumza na HabariLeo kuhusu utekelezaji wa mwongozo huo, Kaimu Mkurugenzi (Elimu) kutoka Wizara ya Tamisemi, Juma Kaponda alisema lengo la kutolewa kwa mwongozo huo ni kuzikumbusha shule zote kuzingatia utekelezaji wa kuwa na mihimili na si zaidi na kuhakikisha wanafunga shule zao kwa mapumziko yote sawa na shule za serikali.

Alisema kwa kuwa shule zote ziko chini ya makatibu tawala na wakurugenzi, ofisi ya Tamisemi inatarajia kuwa viongozi hao watazichukulia hatua shule zitakazobainika kukiuka mwongozo huo.

Alisema lengo la kuanzishwa kwa mwongozo huo ni kuhakikisha elimu inayotolewa nchini haitolewi kwa vipindi vinavyopishana na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu na kupumzika kwa wakati mmoja.

“Zipo shule binafsi ambazo zimekuwa na mihula mitatu na nyingine hadi minne, mwongozo huu unawakumbusha kuwa katika uendeshaji wa shule utaratibu ni mmoja, hakuna shule za binafsi wala za serikali,” alisisitiza.

Alisema pia kulikuwa na baadhi ya mikoa yenye kutofautiana mihula hali iliyosababisha mkanganyiko katika jamii, kwani wakati wanafunzi wengine wakirejea nyumbani kwa likizo wengine ndio wanarejea shuleni.

Alisema utaratibu wa kuwa na mihula miwili si mpya kwani ulikuwepo tangu zamani na hata wamiliki wengi wa shule wanapoenda kusajili shule zao, hupatiwa taratibu nzima za namna ya kuendesha shule hizo.

Alisema kwa mujibu wa mwongozo huo, una mihula miwili yenye vipengele vidogo ndani yake, ambapo shule zinapofunguliwa Januari, hufungwa kwa likizo fupi Aprili, na zinapofunguliwa hufungwa kwa likizo ndefu ya mwezi mmoja, Mei mwishoni.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *