Home / Habari Za Kitaifa / Jenerali Mwamunyange atoa wosia mzito

Jenerali Mwamunyange atoa wosia mzito

ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amewataka Watanzania kuendeleza umoja, mshikamano na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuilinda nchi.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam na wakati wa gwaride la kuwaaga majenerali wastaafu 11 lilolilofanyika Kambi ya Twalipo Mgulani jijini Dar es Salaam.

“Wenzetu watatucheka sana wakiona hii nchi inasambaratika kwa sababu zozote zile za kisiasa, uzembe au namna yoyote, kwa hiyo tushirikiane wote katika kuijenga nchi yetu kwa manufaa ya wananchi,” alisema Mwamunyange.

Mwamunyange pia alitoa rai kwa Jeshi la Polisi kuendeleza uzalendo, nidhamu iliyopo sasa ili kuimarisha weledi na kulifanya jeshi hilo kubaki na sifa.

Jenerali huyo pia alisema pamoja na changamoto zilizokuwepo katika jeshi hilo wakati akiwa kiongozi ikiwamo ufinyu wa bajeti na hivyo kushindwa kukidhi mahitaji yote jeshi liliendelea kuwa na nidhamu umahiri,weledi na kuwa mafano kwa majeshi mengine duniani.

“Kuna wakati mwingine tulikuwa hatuna fedha ya kununua sare za wanajeshi wote muda mwingine tunaishiwa mafuta,” aliongeza Mwamunyange.

Alimuomba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa sasa Jenerali Venus Mabeyo kuendeleza yale mazuri yaliyopo na kujali maslahi ya maofisa na kuangalia kero zao ili kujenga msingi mzuri.

Wengine walioagwa katika gwaride hilo ni pamoja Brigedia Jenerali Sara Rwambali, Brigedia Jenerali Josia Makere, Brigedia Jenerali Methew Sukambi, Brigedia Jeneral Joseph Chengelela na Meja Jenerali Rugashian Laswai.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *